Jumapili 31 Mei 2026 - 14:20
Maonesho Makubwa ya Sanaa Yakiwa na Ujumbe wa Ubinadamu na Umoja Yafanyika Dar es Salaam Tanzania

Hawza/ Katika siku iliyogubikwa na ubunifu, mafunzo, utamaduni na ujumbe wenye kugusa hisia za kibinadamu, maonesho ya sanaa yenye kaulimbiu “Ubinadamu na Umoja” yameacha alama ya kipekee katika mioyo ya washiriki waliohudhuria tukio hilo maalumu.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, Maonesho hayo yaliyoandaliwa na wanafunzi wa Idara ya Sanaa Bunifu ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (BAAD), kwa kushirikiana na Kituo cha Utamaduni cha Iran Tanzania, yalifanikiwa kuwakutanisha wasanii, wanafunzi, wadau wa utamaduni pamoja na wapenda sanaa katika jukwaa moja lenye sura ya elimu, ubunifu na mshikamano wa kiutu.

Tukio hilo lilikuwa ni zaidi ya maonesho ya kawaida ya kazi za sanaa, kwani liligeuka kuwa sehemu ya mawasiliano ya fikra, hisia na tamaduni mbalimbali, ambapo washiriki walipata nafasi ya kujionea uwezo mkubwa wa sanaa katika kuwasilisha ujumbe unaovuka mipaka ya lugha na tofauti za kijamii.

Kupitia kazi mbalimbali zilizobuniwa na wanafunzi, washiriki waliona ubunifu wa hali ya juu uliobeba ujumbe wa maisha, matumaini, utu na mshikamano wa kibinadamu, kila mchoro, kila kazi ya ubunifu na kila mawasilisho yalibeba simulizi ya kipekee iliyolenga kugusa hisia na kuibua tafakuri mpya kuhusu nafasi ya mwanadamu katika jamii.

Aidha, moja ya vivutio vikubwa vya siku hiyo ilikuwa ziara maalumu ya maonesho ya “Shirazis”, ambayo yaliwapa washiriki fursa ya kujifunza na kufahamu zaidi urithi wa kitamaduni na namna sanaa inavyoweza kuhifadhi historia na utambulisho wa jamii.

Washiriki pia walipata fursa adhimu ya kushiriki darasa maalumu la utengenezaji wa animation, ambapo walijifunza mbinu mbalimbali za kisasa za ubunifu wa kidijitali, kipengele hicho kiliwavutia kwa kiasi kikubwa vijana na wanafunzi waliotamani kupanua maarifa yao katika tasnia ya sanaa za kisasa.

Sambamba na hilo, mjadala maalumu kuhusu nafasi ya ubinadamu ndani ya muziki wa Afrika uliandaliwa na kuibua mawazo mapya kuhusu namna muziki unavyoweza kutumika kama chombo cha kuhamasisha amani, mshikamano na kueneza maadili ya kibinadamu katika jamii.

Washiriki walionesha kufurahishwa na kiwango cha ubunifu kilichoonyeshwa katika tukio hilo, huku wengi wao wakibainisha kuwa; sanaa ina nguvu kubwa ya kuunganisha watu kutoka tamaduni na mazingira tofauti kupitia lugha moja ya hisia na ubinadamu.

Tukio hilo pia lilibeba ujumbe wa kina wa mshikamano wa kibinadamu kupitia kumbukumbu maalumu ya wanafunzi mashahidi wa Minab, jambo hilo liligusa hisia za watu wengi na kuwa sehemu iliyowachochea watu kutafakari juu ya thamani ya utu, amani na mshikamano wa jamii.

Kwa ujumla, maonesho ya “Ubinadamu na Umoja” yamedhihirisha kuwa sanaa si tu njia ya kuonesha vipaji, bali pia ni daraja muhimu linalounganisha mataifa, tamaduni na watu kupitia lugha ya ubinadamu inayozungumza moja kwa moja na mioyo ya watu.

Sanaa Yaunganisha Mioyo: Maonesho ya “Through Many Eyes to Humanity” Yavutia Wadau wa Sanaa Dar es Salaam

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha